Proverbs 4:1-9

Hekima Ni Bora Kupita Vitu Vyote

1 aSikilizeni wanangu, mafundisho ya baba yenu;
sikilizeni kwa makini na mpate ufahamu.
2Ninawapa mafundisho ya maana,
kwa hiyo msiyaache mafundisho yangu.
3 bNilipokuwa mvulana mdogo katika nyumba ya baba yangu,
ningali mchanga na mtoto pekee kwa mama yangu,
4 cbaba alinifundisha akisema,
“Yashike maneno yangu yote kwa moyo wako wote;
yashike maagizo yangu na wewe utaishi.
5 dPata hekima, pata ufahamu;
usiyasahau maneno yangu wala usiyaache.
6 eUsimwache hekima naye atakuweka salama;
mpende, naye atakulinda.
7 fHekima ni bora kuliko vitu vyote; kwa hiyo jipe hekima.
Hata ikikugharimu vyote ulivyo navyo, pata ufahamu.
8 gMstahi, naye atakukweza;
mkumbatie, naye atakuheshimu.
9 hAtakuvika shada la neema kichwani mwako
na kukupa taji ya utukufu.”
Copyright information for SwhNEN